Monday, 18 December 2017

RIPOTI YA MRADI WA KUTOKOMEZWA UTUMIKISHWAJI WA WATOTO KWA JAMII YA WAKULIMA YA ZAO LA TUMBAKU KIJIJI CHA MIGUNGUMALO WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA


ARISE II: Mradi wa Kutokomeza utumikishwaji wa watoto kwa jamii wanaojishughulisha na ulimaji wa zao la Tumbaku unaotekelezwa kijiji cha Migungumalo kilichoko wilaya ya Uyui mkoani TABORA – TANZANIA
Mkataba wa kuanza mradi : Tarehe ya kuanza:  22nd May 2017 hadi 15 nd August 2017
Thamani ya Mradi: Tshs 33,484,500/=
Shirika la Spiritual Life In Christ(SLIC) ni shirika la kidini liliosajiliwa mwaka 2002 kama shirika la kijamii.
Dira yetu ni kuona jamii inafanikiwa  kimwili na kiroho  kwa pamoja
Dhima ama Lengo la shirika hili kuhakikisha jamii inaendelea katika nyanja  zote  kupitia fikra za maisha ya kimwili na kiroho  bila ubaguzi wa rangi, dini, jinsi, umri na hali zote za kiubaguzi
Mratibu wa Mradi Ndg Makala Mohamed
 
SLIC imekuwa ikifanya miradi mbalimbali  mashirika ya kitaifa,kimataifa namakamouni mbalimbali tangu kuanzishwa kwake  mwaka 2002  katika miradi ya mazingira, mapambano ya UKIMWI na magonjwa mengine, haki za binadamu, ujasiriamali, kutetea watoto na wanawake, elimu ya demokrasia na uchaguzi, miradi ya elimu na makundi mengine.
Mnamo 22/05/2017 SLIC  ilifanikiwa  kupata ufadhili wa mradi wa chini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) uitwao  Kutokomeza utumikishwaji wa watoto kwa jamii wanaojishughulisha na ulimaji wa zao la Tumbaku uliotekelezwa kijiji cha Migungumalo kilichoko wilaya ya Uyui mkoani TABORA – TANZANIA
MALENGO
1.      Kutoa elimu katika jamii inayohusu tatizo la kutumikisha watoto katika shughuli za uzalishaji wa zao la Tumbaku
2.      Kuwatafuta ama kuwabaini watoto walioathirika na kutumikishwa katika shughuli za Tumbaku mashambani
 
 
WALENGWA/ WAFAIDIKA WA MRADI
1.      WA MOJA KWA MOJA
Wapokeaji wa moja kwa moja walikuwa kama ifuatavyo: -
1. Kutambuliwa umri wa 12-17 = 120
2. Viongozi wa Serikali na Kijiji na kata na kamati za ulinzi za Watoto  (VVCC, VCLC, DSWO, viongozi wa maendeleo ya Kijiji)
3. Viongozi wa kidini
4. Walimu (2).
7. Watu wa kujitolea wa Jumuia na
8. Timu ya Ulinzi ya Watoto Wilaya (DCPT) 5
JUMLA YAO NI 186
Watoto wa Kike walioibuliwa kwenye mradi
 
2.    WASIO WA MOJA KWA MOJA
Wakazi wa Kijiji cha Migungumalo zaidi ya 500 walipata elimu hii kutoka kwa kamati na viongozi wa serikali na wadau waliohudhuria semina ya mradi wetu
Hivyo zaidi ya wanajamii 618 wamefaidika na mradi huu  sawa na lengo la la SLIC katika kutekeleza mradi huu
NJIA ZILIZOTUMIKA KUFANIKISHA MALENGO YA MRADI
1.      Kufanya mafunzo
2.      Kuunda kamati ya kijiji ya kuwalinda na kuwaibua watoto
3.      Kusambaza vipeperushi na tisheti na khanga zenye ujumbe wa mapambano dhidi ya utumikwashi watoto kwenye mashamba ya tumbaku
4.      Mchezo wa mpira
MATOKEO
MATOKEO CHANYA
1.      Uelewa umeongezeka kwa jamii kuhusu madhara ya kutumikisha watoto Mashambani na kujua haki za watoto kwa ujumla hasa suala la kupata elimu, kulindwa, kupendwa na kuthaminiwa
2.      Mwitikio chanya wa walengwa katika kuhudhuria mafunzo haya
3.      Watoto hao 94 waliopatikana waliweza kukusanywa pamoja kwa mahojiano kidogo kukusanya taarifa zao kasha kukabidhi taarifa zao kwenye mamlaka za serikali na shirika lisilo la kiserikali la JIDA kwa kutekeleza mradi wa kuwaendeleza na kuwasaidia.
4.      Wajumbe 38 (28 me, 10 ke) walioelimishwa juu ya Tatizo hili walisaidia kutoa ushirikiano kupatikana kwa watoto 94 (41me, 43ke) walioathirika toka katika jamii za wanaozalisha zao la Tumbaku
5.      Kupata wawakilishi toka vitongoji saba vinavyounda kijiji cha Migungumalo na Baadae kuwaelimisha juu ya tatizo hili.
6.      Wakulima walielewa madhara ya kazi ya watoto
7.      Uundaji wa kamati kupambana na tatizo na sasa ni kazi.
Uelewa wa kujua haki za binadamu kwa watoto na watu wazima kwamba haki za binadamu hasa kwa watoto zinapaswa kulindwa.
Watoto wa kiume walioibuliwa ambao walicheza mpira siku ya mwisho ya mradi kijijini Migungumalo
 
 
 
MATOKEO HASI TULIYOBAINI ENEO LA MRADI
1.    Tuligundua uwepo wa matokeo ya mimba za utotoni kwa wasichana chini ya miaka 18 kwa sababu ya sekta ya tumbaku.
2.    Umasikini kwa jamii ulifanya kuwatumikisha watoto kama nguvu kazi ya kujiingizia kipato
3.     Watoto kujiingiza kwenye matumizi ya  madawa ya kulevya
 Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Asasi ya SLIC Bw. Eric Samuel
4.    Kupoteza mipango ya shule kwa watoto, kuongezeka kwa watoto ambao hawana kukamilisha shule, kuongezeka kwa watoto ambao wanakamaliza masomo bila kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu

CHANGAMOTO
1.      Kulikuwa na changamoto kidogo kutoka kwa viongozi wa kijiji wachache waliotaka kulipwa kiasi kikubwa cha fedha kuliko kile kilichotengwa kwenye bajeti.
2.      Kulikuwa na woga kidogo katika kutoa ushirikiano kwa kuhofia kukamatwa na mamlaka za kisheria kwa waliokuwa wanawatumisha watoto.
3.    Uwepo wa mila mbaya jadi na desturi  zinazoathiri kundi moja au lingine kupata fursa inayostahili kwa maendeleo yake na jamii kwa ujumla
4.    Kutokuwepo na tofauti ya Usawa wa kijinsia ambapo wanaume wanahusishwa zaidi ya wanawake
5.    Kukosekana elimu ya msingi kwa watu wazima ni kikwazo cha maendeleo na mwamko wa kujua haki na wajibu wao katika jamii zao.
MAONI
1.      Elimu hii iendelee zaidi ili Jamii isijisahau ikawatumisha watoto kwa shughuli za kilimo ikiwa ni pamoja na watoto wenyewe kujitambua haki zao za Elimu na afya
2.      Viongozi wa serikali wanapaswa kuelimishwa umuhimu wa miradi hii kwa jamii na umuhimu wa kushiriki kwa nafasi zao kamaviongozi wa serikali eneo la mradi
3.      Elimu ya jinsia ihamasishwe maeneo ya vijijini ili kuondoa mfumo dume na kandamizi na unyanyasaji kwa makundi mengine
4.      Elimu ya afya na afya ya uzazi itolewe na kusisitizwa maeneo ya vijijini ilikupambana na mimba za utotoni na madhara ya magonjwa mengine kwa jamii.
ASANTENI
MRATIBU WA MRADI SLIC.
17/12/2017

WATOTO WALIOKUWA WANATUMIKISHWA KWENYE JAMII YA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU KIJIJI CHA MIGUNGUMALO.



Asasi ya Spiritual Life In Christ (SLIC) ni asasi ya kidini iliyopo mkoani tabora yenye lengo la kuona jamii inafanikiwa kimwili na kiroho  katika Nyanja ya maendeleo.

Asasi hii imekuwa ikifanya miradi mbali mbali ya ikiwemo mapambanio dhidi ya ukimwi, malaria, mazingira, ukatili wa kijinsia, miradi ya nyuki.


Figure 1 Mratibu wa Mradi Bw Makala Mohamed akitoa mafunzo kwenye mradi wa Kutokomeza Utumikishwaji wa Watoto kwenye jamii za wakulima wa Zao la Tumbaku kijiji cha Migungumalo wilaya ya Uyui mkoani Tabora

Akiongea na gazeti hili afisa Mradi huu Bwa Momahed Makala alisema ,mradi huu unalenga kuwaibua watoto waliokosa fursa na haki zao kama watoto kutokana na shughuli za kilimo cha tumbaku katika kijiji cha Migungumalo Wilayani Uyui.

Mwezi Mei , 2017 asasi ya SLIC ilipata fursa ya kufanya mradi wa  Utokomezwajai wa Utumikishwaji wa watoto kwenye Jamii ya wakulima wa zao la Tumbaku katika kijiji cha Migungumalo ulifadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO)  kiasi cha shilingi 33,494,500.00/= kilitolewa ili kutekeleza mradi huo.

Uwepo  wa timu imara ya wafanyakazi wa ILO, SLIC , Viongozi wa serikali, Jamii ya Wakazi wa Migungumalo na uundwaji wa kamati ulipelekea kuibuliwa kwa watoto  94 waliokuwa wakitumikishwa katika mashamba ya tumbaku.


Figure 2 Watoto wakike walioibuliwa kipindicha mradi wa Utokomezwaji wa utumikishwaji kwa watoto kwenye jamii ya wakulima wa zao la tumbaku kijiji cha Migungumalo Uyui-Tabora

 Naye afisa ufuatiliaji na Tathmini wa SLIC Bwa Eric Samuel alisema Kati ya hao 94 walioibuliwa kwenye utumikishwaji wa kilimo cha tumbaku  wavulana ni 62 na wasichana ni 32; Watoto 13 walirejeshwa shuleni na wengine walozidi umri wa kusoma walipatiwa mafunzo  yakiwemo ya useremala, ufundi ujenzi, ufugaji wa kuku, kilimo cha mbogamboga naujasiriamali.


Figure 3 Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Asasi ya SLIC Bw. Eric Samuel

 

Aidha mradi umebaini uwepo wa magonjwa ya macho kwa watoto , ugonjwa wa kifua  na ugonjwa wa ngozi ambao unatokana na kemikali ama madawa yanayotumika katika kuua wadudu kwenye mimea ya tumbaku kuwaathiri baadhi ya watoto hao


Figure 4 Mgeni  Rasmi Bw Mohamed Shauri akiongea siku ya Michezo yaMradi wa Utokomezwaji wa Utumikishwaji watoto kwenye Jamii za wakulima wa zao Tumbaku  kijiji cha Migungumalo Wilayaya Uyui mkoani Tabora

 

Mradi huu ulihitimishwa kwa mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto walioibuliwa kwenye mradi huu katika kijiji cha Migungumalo  ambapo timu A iliifunga timu B 2-1 . Mchezo huu uliongozwa na ujumbe   usemao “Tuseme Hapana kwa Utumikishwaji wa  watoto  na NDIYO kwa elimu bora wa watoto wetu” uliokuwa kwenye jezi za mpira na tisheti pamoja na vitenge  .


Figure 5 Watoto walioibuliwa kwenye mradi wa kupambana na utumikishwaji kweli jamii ya wakulima wa zao la tumbaku kijiji cha Migungumalo Wilaya ya Ujui

Wananchi waliufurahia mradi huu na kuomba uendelee kwenye vijiji vingine ili kuwasaidia watoto kutoka kwenye shughuli za kilimo cha tumbaku.

HAPPY NEW YEAR 2021

 TUNAENDELEA KUHAKIKISA TUNAPAMBANA NA VVU KWA KUELIMISHA JAMII !! UPIMAJI WA HIYARI WA VVU KWENYE MRADI JIJINI ARUSHA, TANZANIA