Monday, 18 December 2017

WATOTO WALIOKUWA WANATUMIKISHWA KWENYE JAMII YA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU KIJIJI CHA MIGUNGUMALO.



Asasi ya Spiritual Life In Christ (SLIC) ni asasi ya kidini iliyopo mkoani tabora yenye lengo la kuona jamii inafanikiwa kimwili na kiroho  katika Nyanja ya maendeleo.

Asasi hii imekuwa ikifanya miradi mbali mbali ya ikiwemo mapambanio dhidi ya ukimwi, malaria, mazingira, ukatili wa kijinsia, miradi ya nyuki.


Figure 1 Mratibu wa Mradi Bw Makala Mohamed akitoa mafunzo kwenye mradi wa Kutokomeza Utumikishwaji wa Watoto kwenye jamii za wakulima wa Zao la Tumbaku kijiji cha Migungumalo wilaya ya Uyui mkoani Tabora

Akiongea na gazeti hili afisa Mradi huu Bwa Momahed Makala alisema ,mradi huu unalenga kuwaibua watoto waliokosa fursa na haki zao kama watoto kutokana na shughuli za kilimo cha tumbaku katika kijiji cha Migungumalo Wilayani Uyui.

Mwezi Mei , 2017 asasi ya SLIC ilipata fursa ya kufanya mradi wa  Utokomezwajai wa Utumikishwaji wa watoto kwenye Jamii ya wakulima wa zao la Tumbaku katika kijiji cha Migungumalo ulifadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO)  kiasi cha shilingi 33,494,500.00/= kilitolewa ili kutekeleza mradi huo.

Uwepo  wa timu imara ya wafanyakazi wa ILO, SLIC , Viongozi wa serikali, Jamii ya Wakazi wa Migungumalo na uundwaji wa kamati ulipelekea kuibuliwa kwa watoto  94 waliokuwa wakitumikishwa katika mashamba ya tumbaku.


Figure 2 Watoto wakike walioibuliwa kipindicha mradi wa Utokomezwaji wa utumikishwaji kwa watoto kwenye jamii ya wakulima wa zao la tumbaku kijiji cha Migungumalo Uyui-Tabora

 Naye afisa ufuatiliaji na Tathmini wa SLIC Bwa Eric Samuel alisema Kati ya hao 94 walioibuliwa kwenye utumikishwaji wa kilimo cha tumbaku  wavulana ni 62 na wasichana ni 32; Watoto 13 walirejeshwa shuleni na wengine walozidi umri wa kusoma walipatiwa mafunzo  yakiwemo ya useremala, ufundi ujenzi, ufugaji wa kuku, kilimo cha mbogamboga naujasiriamali.


Figure 3 Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Asasi ya SLIC Bw. Eric Samuel

 

Aidha mradi umebaini uwepo wa magonjwa ya macho kwa watoto , ugonjwa wa kifua  na ugonjwa wa ngozi ambao unatokana na kemikali ama madawa yanayotumika katika kuua wadudu kwenye mimea ya tumbaku kuwaathiri baadhi ya watoto hao


Figure 4 Mgeni  Rasmi Bw Mohamed Shauri akiongea siku ya Michezo yaMradi wa Utokomezwaji wa Utumikishwaji watoto kwenye Jamii za wakulima wa zao Tumbaku  kijiji cha Migungumalo Wilayaya Uyui mkoani Tabora

 

Mradi huu ulihitimishwa kwa mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto walioibuliwa kwenye mradi huu katika kijiji cha Migungumalo  ambapo timu A iliifunga timu B 2-1 . Mchezo huu uliongozwa na ujumbe   usemao “Tuseme Hapana kwa Utumikishwaji wa  watoto  na NDIYO kwa elimu bora wa watoto wetu” uliokuwa kwenye jezi za mpira na tisheti pamoja na vitenge  .


Figure 5 Watoto walioibuliwa kwenye mradi wa kupambana na utumikishwaji kweli jamii ya wakulima wa zao la tumbaku kijiji cha Migungumalo Wilaya ya Ujui

Wananchi waliufurahia mradi huu na kuomba uendelee kwenye vijiji vingine ili kuwasaidia watoto kutoka kwenye shughuli za kilimo cha tumbaku.

No comments:

Post a Comment

HAPPY NEW YEAR 2021

 TUNAENDELEA KUHAKIKISA TUNAPAMBANA NA VVU KWA KUELIMISHA JAMII !! UPIMAJI WA HIYARI WA VVU KWENYE MRADI JIJINI ARUSHA, TANZANIA